Sunday, November 29, 2009

KARIBUNI


Karibuni nyote katika hii kona ya "MAHANJUMATI", Hapa tutajitahidi kuwaletea mapishi ya vyakula mbali mbali kwa kadiri tutavyojaaliwa.
Karibu uone kwa macho, kujiramba "RUKHSAAA", Karibu uchukue recipes kwa ajili yako binafsi au kwa ajili ya kupikia familia yako na hata biashara "RUKHSAA"
Karibu tuelimishane kwa lile ambalo hulifahamu au hatulifahamu, karibu utoe maoni yako na utupe nawe recipes zako ukipenda kushare nasi, kwani mchele mmoja ila una mapishi mbali mbali.
Karibu tulipendelee "TUMBO", Kama waswahili wanavyosema "Tumbo Muhimu Ndiyo Sababu Likawekwa Mbele"